Monday, January 22, 2018

Waumini wa Dini Ya Kiislamu Watakiwa Kufuata Maagizo Ya Mtume

Waumini wa dini ya kiislamu Tanzania wametakiwa kufuata mafunzo na maagizo ya Mtume ili kuweza kupata dhawabu mbele za Mwenyezi Mungu.

Hayo yamesemwa na  Mufti Mkuu wa Tanzania Abubakar Zuber  alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya Maulidi iliyoandaliwa na Kiwanda cha NIDA textile Mills|(T) ltd NAMERA GROUP OF INDUSTIES.  amabapo amewataka Waumini wa dini hiyo kusikiliza na kufuata kile anachokisema Mtume.

"Nitoe wito kwa Waumini wa dini ya Kiislamu kufuata na kusikiliza kile anachokisema Mtume kwa sababu Mtume amefundisha mambo mbalimbali ambayo yana Maslaha kwa binadamu name ulimwengu wao hivyo yawapasa kuangalia Mtume amewafundisha nini Alisema

Kwa upande wake  Shekh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum ambaye alizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi pamoja na uongozi mzima wa kiwanda cha NIDA amesema hafla hiyo inafanyika kila mwaka na kwamba katika kufanya hivi kunasaidia amani ya nchi kuendelea kupatikana kwani katika kuadhimisha Maulidi hayo wanafanya maombi hasa ya kuombea taifa.

Aidha amewashukuru uongozi wa NIDA pamoja na kuwapongeza kuweza  kuaanda Maulidi hayo kwani kwa kufanya hivyo wanawakumbusha waumini pamoja na watu wa dini zote kutenda mambo yatakayoleta sawabu mbele za Mwenyezi Mungu.

Hafla hiyo imehudhuriwa na wageni mbalimbali Mgeni rasmi akiwa ni Mh. Rais mstaafu wa Awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi, alieambatana na Makamu wa Rais Mstaafu Dkt. Mohammed Gharib Bilali na Viongozi mbalimbali wa dini ya Kiislam .

    Choose :
  • OR
  • To comment
No comments:
Write comments