Wednesday, January 24, 2018

Kama Una Roho Ndogo Ukiisoma Hii Barua ya Dogo Aslay Lazima Chozi lidondoke


"Jina langu ni Aslay Isihack, jina hili alinipa Mama yangu mwenyewe Bi. Mozza kutokana na maisha niliyopita ya Muziki wengi wananifahamu kwa jina la Aslay.

Barua kwa Mama yangu kipenzi pamoja na mashabiki zangu.

Hellow Mama najua unanisikia mwanao tangu uondoke life its so complicated kuliko nilivyodhania, kila kitu kwangu tabu nakosa sana ushauri wako natamani kuongea nawe japo hata siku moja lakini nafahamu kwa mapenzi ya Mola haiwezekani nakuombea kila la heri huko ulipo.

Japo kwasasa nimepata kibinti pacha wako, jina lake nimemuita Mozza I wish ungemuona mmefanana sana. Kuna kitu Mama nataka kukugusia juu ya ndoto yangu bado sana natamani kuwa msanii mkubwa kama Kaka zangu na Dada zangu walionitangulia kwenye Muziki. Ndoto niliyokuwa nakusimulia kila wakati tukila Chakula cha jioni.

Mama Kila kukicha Wananirushia mawe nisifike niendapo. Mawe yote Mama nimeyaokota najengea barabara nifike niendapo, hakuna wakunifuta mimi machozi yangu nalia kilio cha mtu mzima maumivu ndani kwa ndani.

Juzi nilitamani nikupigie simu nikuambie yanayonisibu mwanao, Namba yako haipatikani labda umeweka call busy unaniombea dua njema. Nimuambie nani yanayonisibu ndani ya Moyo wangu juu ya Mziki wangu na maisha yangu?

Mashabiki wangu ndiyo wananipa Ujasiri wa kupambana na kukomaa hivo hivo. Sikufaidika na kile nilichokifanya kwa zaidi ya miaka 15
Hata mimi ukiniuliza ilikuwaje nakosa cha kukujibu Mama nataka tukae kikao cha dharura, tuone ilikuwaje.

I feel inferior, najihisi mnyonge, Nawaza nitaanzia wapi?. I just feel hopless and more hopeless day by day. I dont know. Kila ninaposhika panageuka mwiba mchungu kwangu.
Natamani kujua kama unafahamu nanyanyaswa kisa Muziki wangu .

Kiukweli Mama siwezi kulalamika sanaa maana hata wakati napokuwa mpweke mashabiki zangu huniliwaza kwa kusapoti kazi zangu wamekuwa ndiyo faraja kwangu.

Ndiyo wananifanya niwe jasiri wa kuwatengenezea Muziki mzuri kila kukicha. Sometimes nikiwaza mwanangu ataishije, na familia nitaitunza vipi, bila Muziki?

Natumaini utanijibu basi hata ndotoni Mama kama barua yangu utaipokea.

Nimekukumbuka sana mwanao
Aslay.
Nakupenda Mama.

    Choose :
  • OR
  • To comment
No comments:
Write comments