Monday, January 22, 2018

Kuna wakati mwingine Katika maisha yetu ya kila siku tunasema pesa ndo kila kitu.Ni kweli lakini kuwa na pesa bila wazo mahususi katika matumizi ni sawa na kuzima moto kwa chafya. Unashangaa huo ndo ukweli watu wengi tunapata pesa lakini hatujui tuitumie vipi pesa hiyo ili iweze kujisalisha. zipo sababu nyingi ambazo zinasababisha matumizi mabaya ya fedha.

Pesa hii ina majina mengi hii ni kutokana na mahali husika wapo wanaita pesa ni sababuni ya roho, mtonyo, mapene, ankara  na majina mengine mengi.  Leo katika makala haya nitakwenda kukuelezea juu ya matumizi mabaya ya pesa yanayofanya kila siku tuwe katika hali ya umaskini.
Yafuatayo ndiyo matumizi mabaya ya pesa.

Kutokuwa na mpangilio wa matumizi ya pesa.
Moja ya changamoto kubwa inayowakumba wengi wetu ni kwamba hatuana mapangalio sahihi juu ya matumizi ya fedha. Tupo baadhi yetu ambao hutamani kila kitu ambacho tunakiona mbele yetu na kukinunua hata kama ulikuwa hauna mapngo wa kununua kitu hicho. Tupo baadhi yetu tukiwa tunatembea tukiona hiki na kile ni lazima tununue hiyo siyo nidhamu ya fedha.

Pia kuna baadhi ya watu wakipata mishara utajua tu kwa kuona matumizi yao wanayoyafanya. Kufanya hivo ni Kujirudisha nyuma mwenyewe jambo lamsingi la kufanya juu ya matumizi sahihi ni kuwa na mapagalio mzuri wa pesa nunua kitu ambacho umepanga kununua. Pia Hakikisha ya kwamba kila pesa unayoipata na kuitumia Unaiandika katika daftari lako la kumbumbuka hii itakusaidia kuwa na nidhamu ya matumizi ya fedha maana utakuwa unajua kila faida na hasara ya jambo unalolifanya.

Kukopa pesa ovyo
Hili ndilo kosa kubwa ambao linawaelemea watu wengi sana. Nadhani utakuwa shaidi mzuri ni jinsi gani!  madeni yanavowatesa au yanavokutesa. Wapo baadhi ya watu wanakopa pesa katika taasisi za kifedha lakini hawana elimu ya kutosha juu ya mikopo hiyo hasa katika kuangalia mkopo utakuwa na faida au hasara. Wengi Hawaelewi kuhusiana na mkopo hasa swala zima la kulipa riba.

Utashangaa kwa mfano mtu anakopa shilingi laki tisa na anatakiwa kurudisha milioni moja ndani ya mwezi mmoja.  Kwa kuwa pesa hiyo haukujua juu ya riba hiyo pindi unaposhindwa kuirejesha utajikutana unanguna na wale wanaosema pesa ni shetani.

Maana yangu ni kwamba kukopa sio kubaya ila jaribu kupata elimu ya kutosha juu ya mikopo na jaribu kufanya uchunguzi wa mkopo hasa swala la riba. Jaribu kufanya mlinganisho kutoka taasisi moja na nyingine hii itakusaidia kujua ni mkopo gani unakufaa.

Tukiachana maswala ya mikopo katika mataasisi ya kifedha wapo baadhi ya watu ni wakopaji wazuri kwa watu wengine kama vile nguo, viatu na pesa. Usiwe na madeni ambayo yamezidi kwa kiwango kikubwa kwani kuwa na madeni kwa kiasi kikubwa yanakurudisha nyuma kwa namna moja au nyingine.

    Choose :
  • OR
  • To comment
No comments:
Write comments