Kocha wa Mnchester CIty Pep Guardiola ametinga fainali ya kombe la ligi nchini England (EFL Cup), ikiwa ni fainali yake ya kwanza tangu aanze kufundisha soka nchini humo.
Kikosi cha Pep kimetinga fainali hiyo baada ya ushindi wa jumla wa mabao 5-3 kwenye mechi mbili za nusu fainali dhidi ya timu ya Bristol City FC ambapo mechi ya kwanza Man City walishinda 2-1 kabla ya usiku wa jana kushinda 3-2.
Katika fainali yake ya kwanza Guardiola anasubiri kujua kikosi chake kitakutana na nani kati ya timu za Arsenal na Chelsea ambazo leo usiku zitakuwa uwanjani kucheza mchezo wa pili wa nusu fainali ambapo katika mchezo wa kwanza Arsenal ikiwa nyumbani ilishinda 1-0.
Msimu uliopita Guardiola alimaliza bila kombe kwa mara ya kwanza katika historia yake tangu aanze kufundisha soka, ambapo akiwa Barcelona alichukua mataji 14 katika misimu minne kabla ya kutwaa mataji saba katika misimu mitatu akiwa na Bayern Munich.
Kikosi cha Guardiola ambacho kimepoteza mchezo mmoja tu msimu huu wa EPL dhidi ya Liverpool kinatajwa kuwa katika wakati mzuri wa kuwania mataji mbalimbali ikiwemo EPL, FA, EFL na UEFA.

No comments:
Write comments