Friday, January 26, 2018

Huu ndio ujumbe wa Mh.Lema kwa Jaji Mkuu wa Tanzania


Baada ya Jaji Mkuu wa Tanzania,Prof. Ibrahim Juma kuwataka wanasiasa na viongozi wa serikali wenye mamlaka ya kikatiba na sheria kutoingia utendaji wa Mahakama na kuheshimu Muhimili huo. Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amesema Mahakama ambayo ni imara katika haki inawezaje kukubali kuingiliwa?.

Lema amemwambia Jaji Mkuu huyo kuwa Mahakama inapaswa kujitazama zaidi huku akimueleza kuwa Mahakama ikiyumba taifa limeyumba pia.

“Mh Jaji Mkuu kauli kuhusu wanasiasa na Watendaji wa Serikali kutokuingilia Mahakama ni kauli muhimu kwa wkt huu, lakini Mahakama ambayo ni imara ktk haki inawezaje kukubali kuingiliwa ?Mahakama inapaswa kujitazama zaidi.Mahakama ikiyumba Taifa linayumba,” ameandika Lema kwenye mitandao yake ya kijamii.

Jaji Ibrahimu alisema hayo, January 23 mwaka huu jijini Dar es salaam, wakati akifafanua siku ya maadhimisho ya siku ya sheria nchini yatakayoadhimishwa Februali Mosi Mwaka huu

    Choose :
  • OR
  • To comment
No comments:
Write comments