Alichokisema Isha Mashauzi kuhusu mziki wa Taarabu
Isha amebainisha hayo wakati akitambulisha 'video' yake mpya ya wimbo 'nibembeleze' kwenye kipindi cha 'FRIDAY NIGHT LIVE' (FNL) kinachorushwa na EATV tinga namba moja kwa vijana, baada ya kuwepo minong'ono mingi kwa wapenzi na mashabiki wa nyimbo hizo wakidai huenda muziki huo umekufa, kwa maana hawasikii vijembe vya maneno wanavyopigana wasanii wenyewe kwa wenyewe kama wanavyofanya baadhi ya waimbaji wa muziki wa bongo fleva.
"Taarabu haiwezi kufa, naweza kusema ni muziki mama wa Afrika, Tanzania au hata duniani. Muziki wa taarabu ukipigwa sehemu yeyote kila mtu ataujua fika kwamba hii ni taarabu tofauti na muziki mingine kwa hiyo hauwezi kufa", alisema Isha Mashauzi.
Pamoja na hayo Isha ameendelea kwa kusema "naweza sema tu kwamba labda wanamuziki wa taarabu hawapendi zile kiki ambazo zipo kwa wanamuziki wengine, leo utasikia huyu sijui anatoka na fulani mara yule vile ndiyo mwisho wa siku aachie kazi yake mpya. Hicho kitu kwenye taarabu hamna naweza kutetea hivyo ndiyo maana wanasema hivyo
No comments:
Write comments