Monday, January 22, 2018

Klabu pekee ambayo haijafungwa kwenye ligi kubwa tano barani Ulaya


Baada ya klabu ya PSG na Manchester City kupoteza mechi zao kwenye michezo ya ligi kuu nchini Ufaransa na Uingereza, kwa sasa Barcelona ndio klabu pekee ambayo haijapoteza mchezo hata mmoja kwenye Ligi kubwa tano za soka barani Ulaya .

Tayari kwenye Ligi kuu ya Uingereza (EPL), Ujerumani (Bundesliga), Ufaransa (League 1) na Italia (Serie A) hakuna timu ambayo haijafungwa isipokuwa ni Barcelona pekee kutoka Hispania (La Liga) ambayo haijafungwa hadi sasa.

Jana Barcelona waliendeleza rekodi hiyo kwa ushindi mnono wa goli 5-0 dhidi ya klabu ya Real Betis, ambapo Mshambuliaji Lionel Messi na Luiz Suarez walitupia goli 2 kila mmoja huku Ivan Ractic akifunga goli moja.

Barcelona wamecheza mechi 20 za Ligi Kuu nchini Hispania na kutoa sare michezo mitatu na kushinda mechi 17. Hadi sasa wanaongoza La Liga kwa alama 53 nyuma ya pointi 11 ya klabu ya Atletico Madrid ambao wapo nafasi ya pili.

Hata hivyo rekodi hii ni kwenye michuano ya Ligi Kuu pekee kwani Barcelona tayari wameshafungwa na Espanyol kwenye mchezo wa kwanza wa kombe la mfalme nchini Hispania

    Choose :
  • OR
  • To comment
No comments:
Write comments