Monday, January 22, 2018

Klabu ya Watford yamtangaza rasmi Kocha wake mpya


Klabu ya soka ya Watford ambayo inashiriki ligi kuu ya Uingereza, imemtangaza kocha wake mpya baada ya kumtimua Marco Silva.

Uongozi wa Watford umemtangaza Javi Gracia (47) ambaye ni raia wa Hispania kuwa kocha wao mpya na tayari wamempatia mkataba wa miezi 18 wa kuifundisha timu hiyo.

Kupitia mtandao wao wa Twitter wa timu hiyo umeandika, “| #watfordfc is delighted to announce the appointment of Javi Gracia as the club’s new Head Coach on an 18-month contract.

Gracia amewahi kuzifundisha timu kadhaa ikiwemo Osasuna, Malaga, Rubin Kazan na nyingine.

    Choose :
  • OR
  • To comment
No comments:
Write comments