Kessy apata hofu kisa Mfaransa wa Simba
BEKI wa kulia wa Yanga, Hassan Kessy amesema kuwa, rekodi za kocha mpya wa Simba raia wa Ufaransa, Pierre Lachantre ni nzuri na zinavutia ukizisikia na kuzisoma.
Hata hivyo, Kessy ambaye aliwahi kuitumikia Simba, ameonyesha kuwa na hofu na uongozi wa klabu hiyo kama utampatia uhuru wa kutosha kocha huyo mwenye rekodi ya kuipatia Cameroon Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2000.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Kessy alisema kuwa kama uongozi wa timu hiyo hautabadilika, kocha huyo hakuna chochote atakachokifanya klabuni hapo na badala yake ataonekana hafai kama ilivyokuwa kwa watangulizi wake.
“Nimeisoma rekodi ya kocha huyo ni nzuri lakini kwa Simba ninayoifahamu mimi kama viongozi wake hawatabadilika basi naye anaweza kuondoka kama walivyoondoka makocha wengine waliomtangulia.
“Wamepita makocha wengi wazuri klabuni hapo lakini kwa sababu ya kutowapa uhuru wa kufanya kazi yao ipasavyo, walionekana hawafai, kwa hiyo hata kwa huyu kama wasipobadilika, pia ataonekana hafai,” alisema Kessy.

No comments:
Write comments