Monday, January 22, 2018

Waumini wa Dini Ya Kiislamu Watakiwa Kufuata Maagizo Ya Mtume

Waumini wa dini ya kiislamu Tanzania wametakiwa kufuata mafunzo na maagizo ya Mtume ili kuweza kupata dhawabu mbele za Mwenyezi Mungu.

Hayo yamesemwa na  Mufti Mkuu wa Tanzania Abubakar Zuber  alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya Maulidi iliyoandaliwa na Kiwanda cha NIDA textile Mills|(T) ltd NAMERA GROUP OF INDUSTIES.  amabapo amewataka Waumini wa dini hiyo kusikiliza na kufuata kile anachokisema Mtume.

"Nitoe wito kwa Waumini wa dini ya Kiislamu kufuata na kusikiliza kile anachokisema Mtume kwa sababu Mtume amefundisha mambo mbalimbali ambayo yana Maslaha kwa binadamu name ulimwengu wao hivyo yawapasa kuangalia Mtume amewafundisha nini Alisema

Kwa upande wake  Shekh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum ambaye alizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi pamoja na uongozi mzima wa kiwanda cha NIDA amesema hafla hiyo inafanyika kila mwaka na kwamba katika kufanya hivi kunasaidia amani ya nchi kuendelea kupatikana kwani katika kuadhimisha Maulidi hayo wanafanya maombi hasa ya kuombea taifa.

Aidha amewashukuru uongozi wa NIDA pamoja na kuwapongeza kuweza  kuaanda Maulidi hayo kwani kwa kufanya hivyo wanawakumbusha waumini pamoja na watu wa dini zote kutenda mambo yatakayoleta sawabu mbele za Mwenyezi Mungu.

Hafla hiyo imehudhuriwa na wageni mbalimbali Mgeni rasmi akiwa ni Mh. Rais mstaafu wa Awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi, alieambatana na Makamu wa Rais Mstaafu Dkt. Mohammed Gharib Bilali na Viongozi mbalimbali wa dini ya Kiislam .

Mtoto wa Navy Kenzo awa kivutio kwa watu

MTOTO wa wanamuziki wa kishua wanaounda Kundi la Navy Kenzo, Emannuel Mkono ‘Nahreel’ na Aika Mareale waliompa jina la Gold, amegeuka kivutio kwa watu mbalimbali baada ya wawili hao kuachia picha yake mtandaoni.

Wanamuziki hao ambao ni kapo ya muda mrefu walionesha picha ya mtoto huyo kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii na kusababisha watu wengi kuichua na kuweka katika kurasa wakimsifia.

Mama wa Gold, Aika aliiambia Over Ze Weekend, kuwa anafurahi kuona watu wengi wamefurahishwa na ujio wa mwanaye, jambo ambalo kwao ni baraka kubwa katika safari yao ya kimaisha.

 Aika na Nahreel

Sugu afikishwa kizimbani Leo


Mbeya. Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’  amefikishwa mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya leo Januari 22, 2018 kusikiliza kesi inayomkabili  ya kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli.

Sugu pamoja  Katibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga walifikishwa mahakamani hapo Januari 19, 2018 lakini  mahakama ilizuia dhamana zao na kuwarejesha rumande hadi leo.

Siku hiyo hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama hiyo, Michael Mteite alitoa uamuzi wa kuwarejesha rumande, kwamba kesi hiyo inatakiwa isikilizwe mfululizo kwa muda mfupi na washtakiwa wakiwa wanafika mahakamani hapo wakitokea mahabusu.

“Mahakama hii inataka kusikiliza kesi hii kwa muda mfupi sana, ndani ya wiki moja kuanzia Jumatatu ijayo (leo)  iwe imeamuriwa, hivyo washtakiwa wataendelea kuwekwa mahabusu,” amesema Mteite.

Sugu na Masonga wameshtakiwa kwa kosa la kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli ambayo waliyatoa katika mkutano wa hadhara walioufanya Desemba30 mwaka jana wakiwa viwanja vya Shule ya Msingi Mwenge jijini Mbeya

Klabu pekee ambayo haijafungwa kwenye ligi kubwa tano barani Ulaya


Baada ya klabu ya PSG na Manchester City kupoteza mechi zao kwenye michezo ya ligi kuu nchini Ufaransa na Uingereza, kwa sasa Barcelona ndio klabu pekee ambayo haijapoteza mchezo hata mmoja kwenye Ligi kubwa tano za soka barani Ulaya .

Tayari kwenye Ligi kuu ya Uingereza (EPL), Ujerumani (Bundesliga), Ufaransa (League 1) na Italia (Serie A) hakuna timu ambayo haijafungwa isipokuwa ni Barcelona pekee kutoka Hispania (La Liga) ambayo haijafungwa hadi sasa.

Jana Barcelona waliendeleza rekodi hiyo kwa ushindi mnono wa goli 5-0 dhidi ya klabu ya Real Betis, ambapo Mshambuliaji Lionel Messi na Luiz Suarez walitupia goli 2 kila mmoja huku Ivan Ractic akifunga goli moja.

Barcelona wamecheza mechi 20 za Ligi Kuu nchini Hispania na kutoa sare michezo mitatu na kushinda mechi 17. Hadi sasa wanaongoza La Liga kwa alama 53 nyuma ya pointi 11 ya klabu ya Atletico Madrid ambao wapo nafasi ya pili.

Hata hivyo rekodi hii ni kwenye michuano ya Ligi Kuu pekee kwani Barcelona tayari wameshafungwa na Espanyol kwenye mchezo wa kwanza wa kombe la mfalme nchini Hispania

Ray: Nimeyatoa maisha yangu kwa mwanangu

Ray na mwanaye.

MWIGIZAJI wa kiume wa Bongo Movies, Vincent Kigosi ‘Ray’ amefunguka kuwa, mwanaye aliyezaa na mwigizaji Chuchu Hans aitwaye Jaden amekuwa ndiye maisha yake kwa sababu sasa kila anachokifanya ni kwa ajili yake na amembadilisha maisha kwa kiasi kikubwa.

Ray aliliambia Ijumaa Wikienda kuwa, ameyatoa maisha yake kwa Jaden na anafanya kazi kwa nguvu kwa ajili yake ili baadaye asipate shida kwani hatapenda afanye sanaa kama yeye.

“Maisha yangu nimemtolea mwanangu na ninafanya kazi kwa nguvu zote kwa ajili yake. Sihitaji aje kuwa msanii hata siku moja, nataka asome, afanye kazi nyingine,” alisema Ray

Dalali ameanza ruti kuhamasisha Simba kutwaa Ubing 


MWENYEKITI wa zamani wa Simba, Mzee Hassan Dalali ‘Handsome Boy’, ameanza harakati za kuhamasisha wanachama wa timu hiyo kwa ajili ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu ambapo amepanga kutembelea Tanga na Zanzibar kabla ya mikoa mingine.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Mzee Dalali alisema kuwa tayari ameshaanza kuzunguka katika matawi mbalimbali ya Mkoa wa Dar kwa ajili ya kuhamasisha umoja na mshikamano kwa lengo la kuweza kutwaa ubingwa wa msimu huu.

“Tayari nimeshaanza ziara yangu ya kuzunguka matawi ya nchi nzima, kwa hapa Dar nimeshakwenda kuongea na wanachama wa matawi ya Mabibo na leo (jana) nitakwenda Gongo la Mboto, lengo kubwa ni kuhamasisha umoja na mshikamano wa matawi ambao kama ulitoweka lakini sasa umeanza kuzaa matunda kutokana na ushirikiano wa viongozi wa juu wa timu, nawapongeza sana.

“Hili nimeamua kufanya mwenyewe kwa mapenzi ya timu yangu kwa sababu ni muda mrefu umoja na mshikamano umekuwa kama umepotea lakini wiki ijayo nitakwenda Tanga kisha Zanzibar, ikizingatiwa tulikuwepo kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi, muda mrefu umepita sasa bila ya kuchukua ubingwa lakini kwa mabadiliko chini ya viongozi wangu ambayo wanayafanya, naamini tutafanikiwa na kushiriki michuano ya kimataifa,” alisema Mzee Dala

Humphrey Polepole afunguka kuhusu UKAWA


Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole amesema kuwa hakuna kitu kinaitwa UKAWA kwani mpango huo ulianzishwa na CHADEMA ili kuvitumia vyama vingine kisiasa.

Polepole amesema kuwa kama UKAWA ingelikuwepo hadi leo basi isingetokea baadhi ya majimbo CHADEMA kushindana na CUF ile hali vyama vyote vipo chini ya muavuli wa UKAWA.

“Hakuna kitu kinaitwa UKAWA, hii ilikuwa project ya Chadema ikivitumia vyama vingine, CUF, NCCR na NLD. Kilichobaki ni UKIWA, katika jimbo lililokuwa la CUF leo CDM na CUF wanamenyana,”ameandika Humphrey Polepole kupitia Twitter.

Hata hivyo, kwenye uchaguzi mdogo wa ubunge katika jimbo la Kinondoni CUF kwa upande wa Prof Lipumba imesimamisha mgombea wake huku CHADEMA nao wakisimamisha mgombea wao