Yanga yaifuata Lipuli Iringa
Kikosi cha mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Yanga kimeondoka mjini Mbeya leo alfajiri kwenda Iringa.
Yanga inakwenda Iringa kwa ajili ya mechi yao ya Ligi Kuu Bara dhidi ya wenyeji wake, Lipuli FC.
Mechi hiyo itachezwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Samora mjini Iringa na Yanga wako tayari.
Kocha Msaidizi wa Yanga, Shadrack Nsajigwa amesema wanachotaka ni kupata pointi tatu.
“Mara ya mwisho tulishinda dhidi ya Azam, tunataka kurejea katika mwendo wetu na litakuwa jambo zuri kushinda tena mechi ijayo,” alisema.
Baada ya kushinda dhidi ya Azam FC, Yanga ilikwenda kucheza mechi ya Kombe la Shirikisho dhidi ya timu ya daraja la pili ya Ihefu FC na kushinda kwa mikwaju ya penalti, kipa wake, Youthe Rostand akiwa shujaa kwa kupangua penalti tatu.

No comments:
Write comments