Thursday, February 1, 2018




Mbunge Chadema ahoji madhara ya kuongeza maumbile

Mbunge wa viti maalumu (Chadema) , Suzan Lyimo leo Februari 1, 2018 ameibua mjadala bungeni baada ya kuhoji kama wanawake wanaochoma sindano kwa lengo la kuongeza maumbile yao wanapata madhara yoyote.

Ametoa kauli hiyo wakati akiuliza swali la nyongeza bungeni, kubainisha kuwa miaka ya hivi karibuni kumekuwa na wimbi la wanawake kutumia sindano hizo, kwamba kama Serikali inalijua jambo hilo imechukua hatua gani.

“Naomba kujua iwapo serikali ina taarifa kwamba wapo wanawake wanaotumia sindano kwa ajili ya kuongeza maumbile yao, kama wanapata madhara  Serikali imechukua jukumu gani kukomesha jambo hilo,” amesema Lyimo.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Afya, Dk Faustine Ndugulile amesema sindano hizo zina madhara makubwa mwilini.

Amesema mwili wa binadamu umeumbwa kwa namna ya asili kwa lengo la kujikinga na mambo mengi ikiwemo mionzi.

Amebainisha kuwa Serikali hairuhusu jambo hilo, dawa zote ambazo hazijasajiliwa zinapingwa vita  kwa kuwa zina madhara kwa watumiaji

    Choose :
  • OR
  • To comment
No comments:
Write comments