Shilole ampa onyo Dada wa kazi
STAA wa filamu na Bongo Fleva, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amesema kuwa tangu amekuwa mke halali wa Ashraf Uchebe, haruhusu dada wa kazi ampikie chakula mumewe huyo.
Akizungumza na gazeti hili, Shilole alisema kuwa mastaa wengi wakiingia kwenye ndoa wanajisahau sana kila kitu wanapenda kufanyiwa na mdada wa kazi na ndiyo maana ndoa zao hazidumu.
“Yaani mimi lazima mume wangu ale chakula cha mkono wangu sikubali mdada wa kazi ampikie, ni marufuku kabisa. Nimruhusu, je akinogewa na mapishi ya mkono wake inakuwaje? Chakula napika mwenyewe kuanzia chai mpaka cha jioni,” alisema Shilole. wanavyopakaza
No comments:
Write comments