Dayna atundikwa mimba
Wednesday, February 21, 2018
MREMBO anayekimbiza kwenye Bongo Fleva, Mwanaisha Said ‘Dayna Nyange’
amejazwa kitumbo ndii kinachodaiwa kumpeleka puta na ndiyo sababu ya
kuwa kimya kwenye muziki.
Habari ilizozipata Za Motomoto News ni kwamba mwanamama huyo ana
ujauzito mkubwa ambao umekuwa ukimsumbua na mara nyingi amekuwa
akijificha kwa kuwa hataki watu wengi wajue kama yupo katika hali hiyo.
“Si unajua Dayna alipata mpenzi Mzungu? Nadhani ndiye ameamua kumzalia
na hataki kabisa kumtaja baba kijacho wake kwani hata marafiki zake wa
karibu ametuficha,” alisema rafiki wa Dayna ambaye aliomba hifadhi ya
jina lake.
Hivi karibuni Dayna, kwenye ukurasa wake wa Mtandao wa Kijamii wa
Instagram aliweka picha yake ikimuonesha ujauzito wake ukiwa mkubwa na
mashabiki wake kuanza kumpongeza kwa hatua hiyo.
Za Motomoto News ilimtafuta Dayna na kumuuliza kuhusu ujauzito wake
pamoja na tetesi za kwamba anazaa na Mzungu ambapo alijibu kwa kifupi:
“Sitaki kuzungumzia mambo ya ujauzito wangu na baba kijacho maana ni maisha yangu binafsi.”
No comments:
Write comments