Okwi amvuruga Chirwa Yanga
MSHAMBULIAJI wa Simba, Emmanuel Okwi, ameonekana kumuumiza kichwa straika wa Yanga, Obrey Chirwa ambapo imebainika kuwa ndiye chanzo cha Mzambia huyo kushindwa kuungana na wenzake kwenye safari ya kuelekea Shelisheli kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya St Louis.
Chanzo makini kutoka ndani ya Yanga kimeliambia Championi Jumatano kuwa Okwi ndiye aliyechangia Chirwa ashindwe kwenda Shelisheli baada ya kulazimisha kucheza mchezo wao wa ligi kuu uliopita dhidi ya Majimaji huku akiwa na majeraha ambapo alipanga kuongeza idadi ya mabao ili kumpita Mganda huyo.
Okwi.
“Ukweli ni kwamba Okwi ndiye ambaye amechangia Chirwa kubakia hapa Dar
baada ya kushindwa kwenda Shelisheli kama wenzake ambavyo walifanya kwa
sababu Chirwa alilazimisha kucheza ile mechi na Majimaji huku akiwa
anaumwa.
“Yeye alipanga atumie mchezo ule kama sehemu ya kumzidi Okwi mabao sasa
bahati mbaya ni kwamba baada ya mchezo kumalizika lile jeraha likazidi
kuwa kubwa hivyo kusababisha hadi jina lake litolewe katika wale ambao
wanasafiri kuelekea nchini humo kwa ajili ya mchezo wetu.
“Hata hivyo, sasa hivi bado anatamani kupona haraka kwa kuwa anataka
kurudi uwanjani mapema ili afunge na awe mfungaji bora wa ligi,”
kilisema chanzo hicho.
No comments:
Write comments