Showing posts with label habari. Show all posts
Showing posts with label habari. Show all posts

Friday, May 26, 2017

KAMPALA

KAMPALA, UGANDA: Mkataba wa mradi wa Bomba la Mafuta kati ya Tanzania na Uganda(Intergovernmental Agreement - IGA) umesainiwa leo.

Ujenzi wa bomba hilo la kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga nchini Tanzania lenye urefu wa Kilometa 1,443, uliokadiriwa kugharimu zaidi ya Dola bilioni 3 nukta 55.

Tukio hilo limekuja siku chache baada ya Marais wa Nchi hizo mbili, Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Jamhuri ya Uganda Yoweri Kaguta Museveni, kutia saini tamko la pamoja la kukamilika kwa majadiliano ya vipengele vya mkataba, Ikulu Jijini Dar es salaam.

Hafla ya kutia saini Mkataba huo iliyofanyika katika Hoteli ya Serena, Jijini Kampala, Uganda imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa nchi zote mbili wakiwemo Mawaziri, Makatibu Wakuu, Wanasheria Wakuu wa Serikali, Wakurugenzi na Viongozi wa taasisi mbalimbali zinazohusika katika mradi huo.

Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Hoima-Uganda hadi Tanga Tanzania, unatarajia kusisimua uchumi wa nchi hizo mbili na katika mchakato wa ujenzi wake zaidi ya watu 10,000 wanatarajiwa kunufaika na ajira.

Hivi Karibuni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli aliuelezea mradi huo kuwa ni mkubwa kwakuwa Uganda imegundua shehena kubwa ya mafuta katika eneo la Hoima kiasi cha mapipa bilioni 6 na laki 5 na kwamba Tanzania inatarajia pia kupata mafuta kule ziwa Tanganyika na ziwa Eyasi, ambayo yatapitishwa katika bomba hilo hilo.

Saturday, May 20, 2017

Unguja

Makamu wa Rais Samia Hassan amewasili Unguja, Zanzibar kutoka Dodoma, kesho atazindua kampeni maalum ya "Mimi na Wewe".

Urusi

URUSI wametengeneza SATAN -2.  SATAN 2 Made in russia likionyeshwa live tarehe 27/10/2016,  hili kombora ndio hatari zaidi kwa sasa duniani limetengenezwa kwa Advanced tecnology ni inter-continental lina fika popote duniani kwa muda mfupi tuu kwa kasi ya ajabu,  lina uzito wa zaidi ya tani 100, linabeba mabomu10-15 ya atomic, kombora kama hili moja linaweza kuigeuza majivu nchi yote ya UFARANSA.   Makombora kama haya 54 yanaweza kuiangamiza USA kabisa.  Pamoja na silaha nyingine kali za kivita ndio maana RAISI wa RUSSIA kwa kujiamini kabisa alisema hivi,  " WE HAVE THE BEST ARMY IN WORLD.

Monday, May 15, 2017

TAARIFA

Waziri wa Elimu Professa Joyce Ndalichako amewasimamisha kazi Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TIE, Dr. Kibga na Nicholas Bureta kufuatia makosa kwenye vitabu vya kujifunzia.

BREAKING NEWS


MIX #BREAKING: Rais Magufuli ameivunja Mamlaka ya Ustawishaji CDA Dodoma (+PICHA)

By David King TZA
onMay 15, 2017 COMMENTS

Leo May 15, 2017 Rais Magufuli ameivunja rasmi Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma (CDA) na kuagiza mali na shughuli zote zilizokuwa zikifanywa na CDA zihamishiwe Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma.

Rais ameivunja CDA kwa kutia saini hati ya Amri ya Rais ya kuivunja Mamlaka hiyo Ikulu Dar es Salaam, tukio ambalo limeshuhudiwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Majaliwa, Waziri wa Ardhi William Lukuvi.

Wengine ni Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Antony Mavunde, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana na viongozi mbalimbali wa wizara.

Rais Magufuli amesema ameamua kuivunja CDA na kuhamishia majukumu yake katika Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma ili kuondoa mgongano wa utoaji wa huduma uliokuwa ukisababishwa na vyombo hivyo viwili na pia kuendana na mahitaji ya sasa ambayo yamedhihirisha kuwa hakuna haja ya kuwepo kwa CDA.

Kufuatia uamuzi huo Magufuli pia ameivunja Bodi ya CDA, aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa CDA Eng. Paskasi Muragili atapangiwa kazi nyingine na ameagiza wafanyakazi wote wa Mamlaka hiyo wahamishiwe Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma na ofisi nyingine za Serikali kadiri inavyofaa.

Thursday, May 11, 2017

TANAGA MAFULIKO

ATHARI ZA MVUA: Mbunge Stephen Hilary Ngonyani almaarufu "Prof. Maji Marefu" akiokoa wananchi jimboni kwake Korogwe, Tanga