Tuesday, May 9, 2017

SUDANI

SUDAN KUSINI: Shirika moja la misaada laonya kuwa huenda watu Milioni 6 wakafariki kufuatia ukame katika nchi hiyo na mataifa jirani.

Onyo hili linakuja wakati ambapo jamii ya kimataifa ikipambana kuchangisha dola bilioni 4.4 kuepusha janga kamili.

Umoja wa Mataifa unasema kati ya dola bilioni 4.4 zinazohitajika kufikia mwezi Julai ili kuzuia kufariki kwa idadi kubwa ya watu, ni asilimia 26 pekeyake ya fedha hizo zilizopatikana.

    Choose :
  • OR
  • To comment
No comments:
Write comments