Saturday, May 6, 2017

STEVE NYERERE

Msanii wa filamu, Steve Nyerere, amedai wasanii wa filamu wanashindwa kufanikiwa kutokana na kukosa ushirikiano huku akidai kuna baadhi yao wanajifanya wao ni mungu watu.
Muigizaji huyo amedai hakuna mtu wa nje ambaye ataweza kuja kuikomboa tasnia yao ya filamu isipokuwa wao wenyewe. “Leo hatupo katika umoja, kwanza ili tuweze kufanikiwa mafanikio hayapo ya mmoja mmoja, mafanikio yote duniani yalipita kwa watu ndiyo wewe ukafanikiwa kwa hiyo lazima tukubaliane, tupendane na nyoyo zetu ziwe zimefunguka kwa kufanya vitu vizuri,” Steve alikiambia kipindi cha Enewz cha EATV.
Aliongeza, “Kuna ma-director wazuri zaidi lakini leo wote hawapo, wanachokikosa ni ushirikiano, tunao ma-director wazuri tu, wanaweza wakafanya kitu kizuri tu ‘site’ lakini ushirikiano hawana, kuna watu wanakuwa Mungu watu haiwezekani, haiwezekani kuwa Mungu mtu jamani Mungu ni mmoja tu,” Muigizaji huyo amekuwa akipingana na wasanii wenzake wa filamu walioandamana mwezi mmoja uliopita wakiishinikiza serikali kuzifungia filamu za nje ambazo hazilipi kodi kwa madai zinawaharibia soko lao la filamu za ndani.
.
TOA MAONI YAKO HAPA

    Choose :
  • OR
  • To comment
No comments:
Write comments