RAIS John Magufuli ameagiza kuanzia kesho taasisi zote zinazotoa huduma katika Bandari ya Dar es Salaam ziungane na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA) kutoa huduma kwa saa 24 ili kukabiliana na tatizo la ucheleweshaji wa mizigo bandarini.
Alitoa agizo hilo jana wakati wa akizindua Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) na kuongoza Mkutano wa 10 wa Baraza hilo uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu, Dar es Salaam. “Kama alivyosema Waziri Mkuu, tunataka kufanyia kazi maoni yenu mara moja, kuanzia Jumatatu nataka taasisi zote za pale bandarini zitoe huduma saa 24, haiwezekani bandarini kwetu mizigo ichukue siku 13 kuitoa wakati bandari za wenzetu majirani inatoka baada ya siku tatu, tutashindana vipi?” Alihoji Rais Magufuli. Rais alikuwa akijibu maoni ya wafanyabiashara hao ikiwemo tatizo la ucheleweshaji wa mizigo bandarini na hivyo kuagiza kuanzia kesho taasisi zote katika bandari ya Dar es Salaam na TPA kufanya kazi kwa saa 24. .
TUPIA NENO LA HONGERA WA MH JPM KAMA JAMBO HILI LA BANDARI KUHARAKISHA UMELIPENDA...!!! MATANGAZO NI TSH8,000/=KWA WIKI.
POST 3 KWA SIKU NICHECK DM.
Sunday, May 7, 2017
RAIS JOHN MAGUFULI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Write comments