Saturday, July 29, 2017

NEW VIDEO HARMONIZE SUNA

117K views 6 Hours Ago
#SINA WIMBO  MPYA KUTOKA KWA KIJANA WAKO @HARMONIZE_TZ FUATA LINK HII KWENYE BIO YA @harmonize_tz 👉https://youtu.be/nuLx7gXkt6s KUITAZAMA 🙏

Friday, May 26, 2017

KAMPALA

KAMPALA, UGANDA: Mkataba wa mradi wa Bomba la Mafuta kati ya Tanzania na Uganda(Intergovernmental Agreement - IGA) umesainiwa leo.

Ujenzi wa bomba hilo la kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga nchini Tanzania lenye urefu wa Kilometa 1,443, uliokadiriwa kugharimu zaidi ya Dola bilioni 3 nukta 55.

Tukio hilo limekuja siku chache baada ya Marais wa Nchi hizo mbili, Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Jamhuri ya Uganda Yoweri Kaguta Museveni, kutia saini tamko la pamoja la kukamilika kwa majadiliano ya vipengele vya mkataba, Ikulu Jijini Dar es salaam.

Hafla ya kutia saini Mkataba huo iliyofanyika katika Hoteli ya Serena, Jijini Kampala, Uganda imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa nchi zote mbili wakiwemo Mawaziri, Makatibu Wakuu, Wanasheria Wakuu wa Serikali, Wakurugenzi na Viongozi wa taasisi mbalimbali zinazohusika katika mradi huo.

Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Hoima-Uganda hadi Tanga Tanzania, unatarajia kusisimua uchumi wa nchi hizo mbili na katika mchakato wa ujenzi wake zaidi ya watu 10,000 wanatarajiwa kunufaika na ajira.

Hivi Karibuni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli aliuelezea mradi huo kuwa ni mkubwa kwakuwa Uganda imegundua shehena kubwa ya mafuta katika eneo la Hoima kiasi cha mapipa bilioni 6 na laki 5 na kwamba Tanzania inatarajia pia kupata mafuta kule ziwa Tanganyika na ziwa Eyasi, ambayo yatapitishwa katika bomba hilo hilo.

Saturday, May 20, 2017

Unguja

Makamu wa Rais Samia Hassan amewasili Unguja, Zanzibar kutoka Dodoma, kesho atazindua kampeni maalum ya "Mimi na Wewe".

Urusi

URUSI wametengeneza SATAN -2.  SATAN 2 Made in russia likionyeshwa live tarehe 27/10/2016,  hili kombora ndio hatari zaidi kwa sasa duniani limetengenezwa kwa Advanced tecnology ni inter-continental lina fika popote duniani kwa muda mfupi tuu kwa kasi ya ajabu,  lina uzito wa zaidi ya tani 100, linabeba mabomu10-15 ya atomic, kombora kama hili moja linaweza kuigeuza majivu nchi yote ya UFARANSA.   Makombora kama haya 54 yanaweza kuiangamiza USA kabisa.  Pamoja na silaha nyingine kali za kivita ndio maana RAISI wa RUSSIA kwa kujiamini kabisa alisema hivi,  " WE HAVE THE BEST ARMY IN WORLD.

Monday, May 15, 2017

TAARIFA

Waziri wa Elimu Professa Joyce Ndalichako amewasimamisha kazi Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TIE, Dr. Kibga na Nicholas Bureta kufuatia makosa kwenye vitabu vya kujifunzia.

BREAKING NEWS


MIX #BREAKING: Rais Magufuli ameivunja Mamlaka ya Ustawishaji CDA Dodoma (+PICHA)

By David King TZA
onMay 15, 2017 COMMENTS

Leo May 15, 2017 Rais Magufuli ameivunja rasmi Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma (CDA) na kuagiza mali na shughuli zote zilizokuwa zikifanywa na CDA zihamishiwe Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma.

Rais ameivunja CDA kwa kutia saini hati ya Amri ya Rais ya kuivunja Mamlaka hiyo Ikulu Dar es Salaam, tukio ambalo limeshuhudiwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Majaliwa, Waziri wa Ardhi William Lukuvi.

Wengine ni Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Antony Mavunde, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana na viongozi mbalimbali wa wizara.

Rais Magufuli amesema ameamua kuivunja CDA na kuhamishia majukumu yake katika Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma ili kuondoa mgongano wa utoaji wa huduma uliokuwa ukisababishwa na vyombo hivyo viwili na pia kuendana na mahitaji ya sasa ambayo yamedhihirisha kuwa hakuna haja ya kuwepo kwa CDA.

Kufuatia uamuzi huo Magufuli pia ameivunja Bodi ya CDA, aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa CDA Eng. Paskasi Muragili atapangiwa kazi nyingine na ameagiza wafanyakazi wote wa Mamlaka hiyo wahamishiwe Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma na ofisi nyingine za Serikali kadiri inavyofaa.

Saturday, May 13, 2017

DAVIDO

R.kell afanya rimx nyimbo ya  davido

Thursday, May 11, 2017

TANAGA MAFULIKO

ATHARI ZA MVUA: Mbunge Stephen Hilary Ngonyani almaarufu "Prof. Maji Marefu" akiokoa wananchi jimboni kwake Korogwe, Tanga

Tuesday, May 9, 2017

SIMBA

Banda na Mzamiru wawashukuru mashabiki kwa kuwachagua wachezaji bora wa mwezi.
Habari Kamili click link kwenye Bio

SUDANI

SUDAN KUSINI: Shirika moja la misaada laonya kuwa huenda watu Milioni 6 wakafariki kufuatia ukame katika nchi hiyo na mataifa jirani.

Onyo hili linakuja wakati ambapo jamii ya kimataifa ikipambana kuchangisha dola bilioni 4.4 kuepusha janga kamili.

Umoja wa Mataifa unasema kati ya dola bilioni 4.4 zinazohitajika kufikia mwezi Julai ili kuzuia kufariki kwa idadi kubwa ya watu, ni asilimia 26 pekeyake ya fedha hizo zilizopatikana.

Sunday, May 7, 2017

LUCKY VINCENT

Shule ya #LuckyVincent,  ilianzishwa  31/1/2006 na kusajliwa rasmi mnamo 29/ 12 /2006 kwa namba AR.02/7/E.A 028.
.
.
Katika matokeo ya darasa la saba mwaka 2016 shule hiyo ilishika nafasi ya kwanza (kati ya 331 )  kimkoa na na nafasi ya 20 ( kati ya 8109 ) Kitaifa.
.
.
Jambo hilo lilifanya wazazi wengi kupeleka watoto katika shule hiyo, wengine wakiwahamisha kutoka shule nyingine ili wakafaulu vyema. #CloudsDigital imebaini kwamba darasa la 7 katika shule hiyo lina wanafunzi 106, jambo linaloonyesha kwamba wazazi walijenga imani kwa shule hiyo. Imani ambayo pia ilichangiwa na walimu 2 waliotangulia mbele ya haki wakiwa na wanafunzi wao 32 na dereva.
.
.

ARUSHA

ARUSHA: TANESCO imekata umeme kwa Majeshi ya Ulinzi na Usalama pamoja na Hospitali za Serikali kutokana na malimbikizo ya madeni.
.
Taasisi zilizokatiwa umeme na kiasi wanachodaiwa ni pamoja na Jeshi la Wananchi 'TPDF' (Sh Milioni 538), Makao Makuu ya Polisi Mkoa na vituo vyao (Sh. Milioni 271), Jeshi la Kujenga Taifa JKT-Oljoro(Sh Milioni 57) na Hospitali zote za Serikali (Sh. Milioni 58). .

Kwa mujibu wa Ofisa Uhusiano wa TANESCO wa Mkoa huo amesema kuwa huo ni uetekelezaji wa agizo la Rais Magufuli kuwakatia umeme wadaiwa sugu.

SIMBA

Timu ya soka ya Simba imerejea kileleni mwa ligi baada ya kuisambaratisha African Lyon kwa bao mbili kwa moja.

BARANI URAYA

EPL: Klabu ya Arsenal imeinyuka magoli 2-0 Manchester United hii leo.
.
Magoli hayo yamefungwa na Xhaka(Dakika 54) na Welbeck(Dakika 57).

TANGA

TANGA: Ajali mbaya imetokea usiku huu eneo la Lusanga, Muheza. Basi aina ya Coaster likitokea Tanga kuelekea Korogwe limegonga Lori kwa nyuma na kusababisha vifo vya watu kdhaa (inadaiwa ni karibu gari zima)

NAIBU WAZIRI WILLIAM OLE NASHA

KutokaArusha: Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, William ole Nasha alitoa pole kwa msiba huo kama mzazi kwani msiba huo ni mgumu na mzito kwa jamii.
Naye Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, ambayeshugulikia elimu, Avemaria Semakafu  ambaye anashugulikia masuala ya elimu alikemea tabia ya kuwachafua watoto kwakuingiza imani za kishirikina na kutoa rai kuungana kwa pamoja ili kushirikiana kwa pamoja na kutoa rai kwa uongozi wa Jiji la Arusha kutoa mafunzo maalum ya saikolojia kwa watoto hawa waliobaki shuleni ili waweze kuondoa mawazo ya taswira ya jinsi ajali ilivyotokea.
Alitoa angalizo kuwa ajali nyingi sana zinaweza kuzuilika endapo madereva watakuwa makini barabara inatumiwa na watu wengi na ninahakika gari hili lilikuwa na nwendokasi hivyo madereva kuweni waangalifu.
Alisisitiza kuwa siwezi kusema dereva huyu alikuwa mbovu hapana lakini umakini unahitaji pia madereva mzingatie hali ya hewa.

RAIS JOHN MAGUFULI

RAIS John Magufuli ameagiza kuanzia kesho taasisi zote zinazotoa huduma katika Bandari ya Dar es Salaam ziungane na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA) kutoa huduma kwa saa 24 ili kukabiliana na tatizo la ucheleweshaji wa mizigo bandarini.
Alitoa agizo hilo jana wakati wa akizindua Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) na kuongoza Mkutano wa 10 wa Baraza hilo uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu, Dar es Salaam. “Kama alivyosema Waziri Mkuu, tunataka kufanyia kazi maoni yenu mara moja, kuanzia Jumatatu nataka taasisi zote za pale bandarini zitoe huduma saa 24, haiwezekani bandarini kwetu mizigo ichukue siku 13 kuitoa wakati bandari za wenzetu majirani inatoka baada ya siku tatu, tutashindana vipi?” Alihoji Rais Magufuli. Rais alikuwa akijibu maoni ya wafanyabiashara hao ikiwemo tatizo la ucheleweshaji wa mizigo bandarini na hivyo kuagiza kuanzia kesho taasisi zote katika bandari ya Dar es Salaam na TPA kufanya kazi kwa saa 24. .
TUPIA NENO LA HONGERA WA MH JPM KAMA JAMBO HILI LA BANDARI KUHARAKISHA UMELIPENDA...!!! MATANGAZO NI TSH8,000/=KWA WIKI.
POST 3 KWA SIKU NICHECK DM.

Saturday, May 6, 2017

MVUA KUBWA YANYESHA TANGA

KOROGWE, TANGA: Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha wilayani hapo zimesababisha kifo cha Mama na Mtoto wake. Wengine 8 wajeruhiwa.

Kati ya majeruhi hao mmoja mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja.

WANANCHI WAKIWA WAKIWA ENEO LA SHULE


Sehemu ya wananchi wakiwa katika eneo la Shule ya Lucky Vincent iliyopo mkoani Arusha kwa ajili ya kufuatilia taarifa zaidi juu ya ajali iliyohusisha gari aina ya Coaster iliyokuwa imebeba wanafunzi wa shule hiyo.

Endelea kufuatilia page zetu  kutazama @salimbizz  kwa taarifa zaidi.

#CMG inatoa pole kwa msiba huu mzito.

STEVE NYERERE

Msanii wa filamu, Steve Nyerere, amedai wasanii wa filamu wanashindwa kufanikiwa kutokana na kukosa ushirikiano huku akidai kuna baadhi yao wanajifanya wao ni mungu watu.
Muigizaji huyo amedai hakuna mtu wa nje ambaye ataweza kuja kuikomboa tasnia yao ya filamu isipokuwa wao wenyewe. “Leo hatupo katika umoja, kwanza ili tuweze kufanikiwa mafanikio hayapo ya mmoja mmoja, mafanikio yote duniani yalipita kwa watu ndiyo wewe ukafanikiwa kwa hiyo lazima tukubaliane, tupendane na nyoyo zetu ziwe zimefunguka kwa kufanya vitu vizuri,” Steve alikiambia kipindi cha Enewz cha EATV.
Aliongeza, “Kuna ma-director wazuri zaidi lakini leo wote hawapo, wanachokikosa ni ushirikiano, tunao ma-director wazuri tu, wanaweza wakafanya kitu kizuri tu ‘site’ lakini ushirikiano hawana, kuna watu wanakuwa Mungu watu haiwezekani, haiwezekani kuwa Mungu mtu jamani Mungu ni mmoja tu,” Muigizaji huyo amekuwa akipingana na wasanii wenzake wa filamu walioandamana mwezi mmoja uliopita wakiishinikiza serikali kuzifungia filamu za nje ambazo hazilipi kodi kwa madai zinawaharibia soko lao la filamu za ndani.
.
TOA MAONI YAKO HAPA

ALICHO SEMA BARAKA LEO KWENYE PAGE YAKE YA INSTAGRAM

Tangu nazaliwa sijapata kuona Nchi yenye wajuaji wengi kama #TANZANIA..tangu nazaliwa sijawai kupata kuona Nchi yenye binadamu wenye chuki baada kuona mtu kafanikiwa kama #TANZANIA siku hizi mashabiki wamekuwa walimu wa mashahiri na wamekuwa wajuaji kuliko hata sisi tunaoimba mziki...@Darassacmg katoa wimbo wake mpya... ni wimbo mkali sana sio audio tu..adi video @hanscana_ umeuwa lakini kuna izi page zinazojihita page za udaku siku hizi...zinaboa sana naona kuna kitu wanapost sijui waga wanatumiana hili kurudisha mafanikio ya watu nyuma...Ujue mziki sio kitu ki lahisi kama watu wengi humu ndani  mnavyodhania na sio lazima kila kitu kiwe sawa au mapokezi kufanana na kilichopita nyuma...Hakuna kitu kinaboa Duniani kama mtu unapoteza muda wako na nguvu nyingi kuwekeza katika kazi yako au kupigania mafanikio yako,alafu kinakuja kijimtu sijui hata kimetoka wapi kinaanza kuponda kile kitu ulichopoteza muda na nguvu nyingi na pesa pia Nyie watu wajuaji mnaboa kinoma...Tungeni zenu Nzuri na video zenu Nzuri tuzione,Hao Hao kesho ndio utawasikia wakiimba kama wimbo wa taifa.... Oy mwanangu @Darassacmg congratulation my brother ngoma kali kinoma tena video ndio umeuwa kabsaaaaaaaaaaaaaaaaaaa #HASARAROHO link kwa bio ya @Darassacmg

NAY WA MITEGO ATAFANYA SHOW KUBWA DAR LIVE

#WapoTour nizamu ya #DarLive  Njoo wewe na yule Njooni Tuvunje Kibubu na Mrlover @naytrueboy #babayaga Shika iyo Th. 2o/05/2017 #Wapooooooo

Wimbo mpya Wa darasa umedhihirisha kuwa ile ngoma ya Muziki alibahatisha

Darasa ametoa ngoma mpya ambayo kwa kweli imedhihirisha kuwa msanii huyu hana kipaji cha kutunga mashairi mazuri. Si hivyo tu ngoma hii imetoa picha kuwa msanii huyu siyo mbunifu kwani ngoma hiyo inaelekea kufanana na ngoma ya muziki

Video kali sana ila audio kuna muda nahisi nasikiliza Muziki....